Share
Go down
avatar
Posts : 1
Join date : 2018-07-14
View user profile

Namna ya Kulipa kwa Kutumia Mfumo wa Kielektroniki

on Tue Jul 17, 2018 11:14 am
THE INSTITUTE OF FINANCE MANAGEMENT

TAARIFA KWA UMMA
Jumuiya ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) pamoja na Umma kwa ujumla mnataarifiwa kuwa kuanzia mnamo mwezi Januari 2018 malipo yoyote kwa ajili ya huduma mbalimbali zitolewazo na Chuo yamekuwa yakifanyika kwa njia ya Kielektroniki kupitia mfumo ulioanzishwa na serikali ujulikanao kama Government e-Payment Gateway.

Kwa sababu hiyo, Wanafunzi pamoja na wadau mbalimbali wanatakiwa, kabla ya kufanya malipo kwa Chuo, wapate namba ya malipo (control number) kutoka kwenye mfumo wa taarifa za Mwanafunzi (Student Information System) kwa Wanafunzi ama kutoka kwenye mfumo wa malipo (Payment Portal) kwa wale wasio wanafunzi.
Namna ya Kulipa kwa Kutumia mfumo wa Kielektroniki (Government ePayment Gateway).
Malipo kwa ajili ya Ada (Kwa Wanafunzi tu)
1. Ingia kwenye mfumo wa taarifa za mwanafunzi  (Student Information System Portal
2. Fungua akaunti yako ya SIS 3. Bofya sehemu iliyoandikwa ‘Fee Payments’  ili uweze kupata namba yako ya malipo (control number) 4. Nakiri namba yako ya malipo (control number) na kisha tembelea mojawapo ya Benki zifuatazo kwa ajili ya kulipia (CRDB, NBC, TPB na NMB)
Back to top
Permissions in this forum:
You cannot reply to topics in this forum